Full-Width Version (true/false)


Watanzania Watakaowasaidia Wahamiaji Haramu Kukiona

Na Ahmad Mmow, Lindi.
KATIKA kuhakikisha wahamiaji haramu hawapati nafasi ya kuingia nchini.Kamishina  jenerali wa uhamiaji, Dkt Anna Makakala amewaasa wananchi wasishiriki kuwapahidhi na   kuwasafirisha wahamiaji haramu.

Dokta Makakala ametoa onyo hilo jana, wakati anahitimisha ziara yake ya kikazi ya siku mbili aliyoifanya mkoani.Ambapo  alizungumza na watumishi wa idara hiyo, ikiwa pamoja na kusikiliza changamoto mbalimbali kutoka kwa watumishi hao.

Alisema idara ya uhamiaji iko makini kufuatilia kila kona ili kuwabaini wananchi wanaoshirikiana na wahamiaji na kwamba pindi watakapo wabaini sheria kali zitachukuliwa  dhidi yao.

“Sheria ya uhamiaji kwa sasa imeongezewa makali , mtu atakaejihusisha na shughuli hiyo basi atatozwa faini isiyopungua sh. Milioni 20 Au kifungo cha miaka 20 au vyote kwa pamoja.Ikiwa ni pamojana kutaifisha mali zote zitakazohusika kuwasafirisha wahamiaji hao,"alisema kamanda Dkt Makakala

Awali akisoma taarifa ya utendaji kazi ya uhamiaji kwa Mkoa wa Lindi Afisa uhamiaji mkoa ,Abdallah Katimba alisema kutokana na doria zinazofanywa  mara kwa mara katika nyumba za kulala wageni, vituo vya mabasi, bara bara kuu ya Dar-es-salaam- Mtwara na njia za michepuko zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia na kupitia ndani ya Mkoa  wa Lindi na kuelekea nchi za kusini mwa Afrika waliweza kukamata raia wawili wa Vietnam,watano wa Ethiopia na rmmoja wa Malawi.

Hata hivyo Katimba alisema kuwepo kwa Mkoa wa Lindi katika mwambao wa bahari ya Hindi pamoja na kuwa jirani na nchi ya Msumbiji kumesababisha raia wengi wa Msumbiji kuingia  chini na kulowea  kwasababu za  kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.

Alisema kwa kushirikiana na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) katika utowaji wa vitambulisho vya taifa , kwa lengo la kuwabaini wahamiaji haramu ambalo linaendelea hadi sasa, jumla ya watu 8,123 wasio raia wa tanzania wamebainika kupitia ofisi ya uhamiaji ya mkoa na wilaya zilixipo mkoani humu.

No comments

Powered by Blogger.