Waziri Kairuki Akutana Na Shirikisho La Madini La Nchini India
Waziri
wa Madini, Angellah Kairuki amekutana Wawekezaji kutoka Shirikisho la
Madini ya Granite la nchini India (Federation of Indian Granite &
Stone Industry) ambao wameonesha nia ya kuwekeza kwenye Sekta ya
Uongezaji Thamani Madini ya Mawe yenye thamani ya Granite na Mable.
Akizungumza
katika kikao kilichofanyika leo tarehe 18 Julai, jijini Dar es Salaam,
Waziri Kairuki ameueleza ujumbe huo kuhusu adhma ya Tanzania
kukakaribisha wawekezaji katika ujenzi wa vinu vya kuyeyusha madini ya
metali, usonara pamoja na ukataji na ung’arishaji madini ya vito hususan
madini ya Tanzanite ambayo kwa kiasi kikubwa yamekua yakisafirishwa nje
ya nchi yakiwa ghafi.
“
Sheria yetu ya Madini ya Mwaka 2010 na Marekebisho yake ya mwaka 2017,
imekataza usafirishaji wa Makinikia pamoja na madini ghafi nje, ndiyo
maana tunakaribisha wawekezaji kwa ajili ya kuwekeza kwenye uongezaji
thamani madini ndani ya nchi,” amesema Waziri Kairuki.
Pia,
Waziri Kairuki amewashauri wawekezaji hao kukutana na Shirika la Madini
la Taifa (STAMICO) ili kuona namna bora ya kushirikiana katika miradi
mbalimbali ikiwemo ya mawe yenye thamani, bati na madini mengine.
Vilevile,
Waziri Kairuki amelitaka shirikisho hilo kuona namna ambavyo linaweza
kushirikiana na wachimbaji wadogo wa madini nchini hususan katika
masuala ya masoko na mitaji.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Shirikisho la Madini ya Granite na Sekta ya
Mawe la nchini India, Keshava Murthy, amemweleza Waziri Kairuki kuwa,
shirikisho hilo liko tayari kuwekeza kwenye madini ya granite pamoja na
marble kwa kuanza na makontena kati ya 20-50 kwa mwezi.
Pia,
Murthy ameongeza kuwa, Shirikisho hilo lina wanachama zaidi ya 1200
ambao wanajihusisha na shughuli za uongezaji thamani madini ya granite
nchini humo.
Kuhusu
ushirikiano na STAMICO, Murthy amemwahidi Waziri Kairuki kuwa,
shirikisho hilo litakutana na shirika hilo kwa lengo la kubadilishana
ujuzi ikiwemo kuangalia namna bora ya kushirikiana katika sekta husika.
Aidha,
amemweleza Waziri Kairuki kuhusu maonesho ya mawe yenye thamani
yanayojulikana kama STONA FARE ambayo huandaliwa na shirikisho hilo na
kuongeza kuwa, ni miongoni mwa maonesho makubwa duniani.
Mbali
na kukutana na Waziri Kairuki, wawekezaji hao wanatarajia kuendelea na
ziara jijiji Dodoma ambapo wanatarajia kukutana na na Shirikisho la
Wachimbaji wa Madini Tanzania, kutembelea Taasisi ya Jiolojia na Utafiti
wa Madini Tanzania (GST) pamoja na kutembelea baadhi ya maeneo yenye
uchimbaji wa Granite jijini Dodoma.
Kabla
ya kuja nchini, wawekezaji hao walitembelea nchi za Namibia, Zimbabwe
na Malawi kwa lengo la kutafuta fursa za uwekezaji kwenye madini hayo.
Kikao
hicho pia, kimehudhuriwa na Mwakilishi kutoka Taasisi ya Uwekezaji
Tanzania (TIC), Wataalam kutoka Wizara ya Madini wakiongozwa na Kaimu
Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Mashariki Mhandisi Ally Maganga
aliyemuwakilisha Kamishna wa Madini.
No comments