Full-Width Version (true/false)


Yanga kukwea pipa leo tayari kuwamaliza Gor mahia kombe la shirikishoKikosi cha klabu ya Yanga kinatarajiwa kuondoka leo jijini Dar es Salaam kuelekea NNairobi, Kenya kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga itakuwa ina kibarua Jumatano ya wiki hii cha michuano hiyo dhidi ya Gor Mahia FC ukiwa ni wa mkondo wa kwanza.

Mechi ya mwisho Yanga kucheza kwenye kundi lake ilikuwa dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kwenda sare ya suluhu tasa ya mabao 0-0.
 
Yanga inaenda kumenyamana na Gor Mahia ikiwa na ina alama moja pekee ambayo iliipata dhidi ya Rayon kutokana na kupoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya MC Alger ya Algeria kwa idadi ya mabao 4-0.

Mchezo huo kwa Yanga utakuwa ni kuhakikisha inapata alama ili kuanza kujiwekea mazingira mazuri ya kusonga mbele kuelekea hatua nyingine.

Katika Kundi D, MC Alger inaongoza ikiwa na alama 4 ikifuatiwa na Gor Mahia yenye 2, na Rayon Sports ikiwa na mbili wakati Yanga ikiwa na 1 pekee.

No comments

Powered by Blogger.