Full-Width Version (true/false)


Yanga SC wanasa kifaa kipyaKlabu ya Young Africans imefanikiwa kumsajili kiungo mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Mohammed Issa Banka kwa mkataba wa miaka miwili.

Yanga imeingia kandarasi na Banka ikiwa sehemu ya maandalizi ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo inawakabili kwa sasa.

Mabingwa hao wa kihistoria wa ligi kuu soka Tanzania Bara ambao wametwaa taji hilo mara tatu mfululizo wamefanikiwa kukamilisha usajili huo baada ya kupita siku kadhaa kuwaongezea mikataba wachezaji wake, beki wa kulia Juma Abdul na mlindalango wake Beno Kakolanya huku wakimrejesha kiungo wao, Deus Kaseke kutoka Singida united.

Wanajangwani hao kwa sasa wapo kambini wakijifua kabla ya kuwakabili Gor Mahia mchezo wa kombe la shirikisho utakao pigwa nchini Kenya.

No comments

Powered by Blogger.