Full-Width Version (true/false)


Yanga yaongezewa watatu wa kimataifa

SHIRIKISHO la Soka Tan­zania (TFF), limepanga kuongeza idadi ya wachezaji wa kimataifa kwa klabu za Ligi Kuu Bara kutoka saba na kufi­kia kumi katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.


Hiyo itakuwa nafasi pekee kwa klabu kongwe za Simba na Yanga ambazo zimekuwa zikilalamikia kubanwa usajili wa profesheno wachache hapo awali.


Simba tayari hadi hivi sasa ina wachezaji nane wa kimataifa ambao ni James Kotei, Emmanuel Okwi, Asante Kwasi, Nicholas Gyan, Haruna Niyonzima, wengine wal­iowasajiliwa hivi karibuni ni Pascal Wawa, Meddie Kagere na Fabrice Kakule.


Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatano, shirikisho hilo limepanga kuanza kutumia kanuni hizo katika msimu ujao wa ligi ili kuhakikisha wawak­ilishi wa michuano ya kimataifa wanakuwa na kikosi cha wachezaji wengi profesheno wenye uzoefu.


Mtoa taarifa huyo alisema, wakati shirikisho hilo likitangaza kuongeza idadi hiyo ya wachezaji tayari limetoa sharti la kutumia nyota saba pekee katika kila mchezo wa ligi huku mashindano ya kimataifa likiwaruhusu kutumia wowote watakaohitaji.


“TFF limepanga kuongeza idadi ya wachezaji wa kimataifa kutoka wachezaji saba hadi kumi katika kuelekea msimu ujao wa ligi.


“Tayari klabu zimeanza kupewa taarifa za usajili huo wa wache­zaji wa kimataifa, lengo kubwa ni baadhi za klabu kuziimarisha timu zao katika kuelekea michuano ya kimataifa.


“Kanuni hizo za wachezaji kumi ziliwahi kutumika misimu mitano iliyopita ya ligi kwa TFF kutoa na­fasi ya kusajili idadi hiyo ya wache­zaji ambayo tunaamini siyo ngeni,” alisema mtoa taarifa huyo.


Alipotafutwa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao, kuzungumzia hilo simu yake ya mkononi iliita bila ya mafanikio ya kupokelewa, lakini Championi linafahamu tayari viongozi wa klabu wameshapewa taarifa.

No comments

Powered by Blogger.