Full-Width Version (true/false)


Yanga yasubiri muujiza kuiua Gor MahiaYanga itakuwa na kibarua kigumu mbele ya Gor Mahia katika mchezo wake wa Kombe la Shirikisho Afrika keshokutwa Jumatano jijini Nairobi Kenya.
Yanga inayoshikiria mkia katika Kundi D haijashinda mchezo wote hivyo wamekwenda Nairobi leo wakiwa na lengo moja tu la kushinda ili kurudisha matumaini yake ya kufanya vizuri katika hatua ya makundi.
 Hata hivyo ndoto yao ya kupata ushindi katika mchezo huu inakuwa ngumu kutokana na maandalizi yao.
Yanga tangu iliivyomaliza mechi ya mwisho katika mashindano ya SportPesa hawajacheza mchezo wowote ya kimashindano na huku timu yao kuvurugika kwa sababu mbalimbali.
Wachezaji wengi wa Yanga wa kikosi cha kwanza walipewa likizo walivyotoka Kenya kwenye mashindano ya SportPesa na wengine mpaka sasa wamegomea kurudi kujiunga na timu kwa sababu ya madai yao mbalimbali.
Uongozi wa Yanga ulizungumza na baadhi ya wachezaji ambao walikubali kuripoti kambini na kuanza mazoezi ya kujiandaa na mechi ya Gor Mahia na si zaidi ya wiki mbili bila hata kucheza mechi yoyote ya kirafiki ya ushindani.
Yanga walikuwa wakaweke kambi Arusha kama benchi la ufundi lilivyopendekeza kwa ajili ya kupata muda wa kutosha kujiaandaa, kuzoa hali ya hewa na mambo mengine muhimu.
Kambi hiyo ilishindikana kutokana na kukosa fedha ambayo wangeweza kuishi Arusha kwa muda wa wiki mbili chini ya kocha Mwinyi Zahera.
Kukosekana kwa wachezaji wengi nyota wa kikosi cha kwanza ambao walicheza mechi mbili za mwanzo dhidi ya USM Alger walifungwa 4-0 na ile waliopata suruhu na Rayon Sport ya Rwanda ni miongoni mwa sababu ambayo itachangia Yanga kutofanya vizuri.
Baadhi ya nyota wa kikosi cha kwanza walikuwa katika mechi mbili za mwanzo na watakosekana ni Obrey Chirwa, Kelvin Yondan, Thaban Kamusoko na wengine.
Nyota wengi wa kikosi cha kwanza ambao ni wachezaji wa kutumainiwa hawapo fiti kulingana na mechi ilivyo na nafasi ya kuisaidia timu kushinda itakuwa ndogo ingawa soka linamatokeo matatu.
Yanga pia walifanya usajili wa dirisha dogo wa Shirikisho la soka Afrika CAF ambapo walitakiwa kuongeza wachezaji watatu ambao ni Mrisho Ngassa, Deus Kaseke na Heriter Makambo, lakini walichelewa kufikisha usajili hao.
Kwa maana hiyo nyota hao watatu hawatatumika katika mechi hiyo licha ya Yanga kama wangewapa wachezaji hao wangeongeza nguvu haswa katika safu yao ya ushambuliaji. 
Wakati Yanga mambo yakionekana kwenda mlama wapinzani wao Gor Mahia mambo ni safi kwani wametoka kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu ya Kenya.
Gor Mahia mbali ya kuchukua ubingwa wa Kenya lakini wameweza kuchukua ubingwa wa SportPesa wakizifunga timu za Tanzania Singida United na Simba katika mechi ya fainali.

Mbali ya hivyo Gor Mahia wametoka kucheza mashindano ya Kagame Cup na kumaliza katika nafasi ya tatu kwa kumfunga JKU mabao 2-0 wao waliondolewa katika nusu fainali dhidi ya Azam.
Ni wazi timu ambayo imetoka katika mashindano inakuwa na hali ya kushindana na faida kwa benchi la ufundi kwa kutambua makosa waliyoyafanya katika mashindano yaliyopita ili yasijitokeze katika michuano mingine.
Kocha wa Gor Mahia, Dylan Kerr ni mzoefu wa soka la Tanzania kwani alishafundisha Simba, wakati kocha wa Yanga, Mwinyi Zahare ndio kibarua chake cha kwanza.

No comments

Powered by Blogger.