Full-Width Version (true/false)


Yemi Alade ajitamba, asema hakuna msanii anaefanya vizuri Nigeria

Staa maarufu kutokea Nigeria Yemi Alade amefunguka kupitia mahojiano aliyoyafanya na radio ya Hot 93.7 Lagos,Nigeria baada ya kuulizwa ni msanii gani Nigeria anashika nafasi ya kwanza kwa sasa? Yemi Alade alijibu kuwa hakuna msanii namba moja kwa sasa.

Yemi Alade amefunguka na kusema kuwa anaheshimu wasanii wote wanaofanya muziki na pia yeye ni shabiki wa kwanza kwenye kazi za Wizkid pamoja na Davido, kupitia mahojiano hayo aliongeza na kusema kuwa wanachofanya Davido pamoja na Wizkid hata yeye anafanya.

Yemi Alade alisema “Kiwango cha mashabiki anachojaza Wizkid hata mimi najaza na pia kiwango hichohicho anachojaza Davido hata mimi najaza kwahiyo wote tunajaza hivyo hakuna msanii namba moja”

No comments

Powered by Blogger.